Ticker

6/recent/ticker-posts

Umuhimu wa Maombi.

Umuhimu wa maombi katika maisha yetu ya kila siku


Maombi ni nguzo kuu ya maisha ya mwanadamu, chanzo cha nguvu za kiroho, silaha ya ushindi, na daraja linalomuunganisha mwanadamu na Mungu. Kuanzia manabii katika Agano la Kale hadi kwa Yesu Kristo katika Agano Jipya, Biblia inaonyesha wazi kuwa miujiza, maajabu, ushindi na majibu ya changamoto yalitokea kupitia sala na maombi.





Mambo muhimu Biblia inaonyesha kupitia maombi,

  • Maombi huleta nguvu
  • Maombi huleta majibu
  • Maombi hubadilisha mazingira
  • Maombi humbadilisha mtu

📖 Yakobo 5:16
“Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana akiomba kwa bidii.”





Yesu kristo Ingawa alikuwa Mwana wa Mungu,aliishi maisha ya maombi siku zote.

1️. Aliomba kabla ya kufanya maamuzi makubwa

📖 Luka 6:12
Alikesha usiku kucha akiomba kabla ya kuchagua mitume 12.

Hivyo kabla ya maamuzi makubwa haijalishi ni aina gani ya maamuzi katika Maisha yako ya kila siku inakupasa kuomba.

2️.Aliomba kabla ya miujiza

📖 Yohana 11:41-43
Kabla ya kumfufua Lazaro, Yesu aliinua macho mbinguni akaomba.

Kila unapomuhitaji Mungu akutendee jambo katika Maisha usiache kuomba na kusali.

3️.Aliomba katika mateso

📖 Luka 22:44
Katika bustani ya Gethsemane, ali
omba kwa bidii.

Haijalishi unapitia magumu kiasi gani katika Maisha usiache kuomba, sala ndio nguzo itakayokuvusha katika hali unayopitia.


Nguvu katika maombi

1️.Nabii Eliya – Mvua ilinyesha kwa maombi

📖 1 Wafalme 18:42-45

Eliya aliomba mara saba ndipo wingu dogo likaonekana, na mvua kubwa ikanyesha.

Hii inafundisha:

  • Uvumilivu katika maombi
  • Kutokukata tamaa
  • Kuendelea hata kama huoni dalili






2️.Danieli – Ushindi katikati ya vitisho

📖 Danieli 6:10

Danieli aliendelea kuomba licha ya amri ya kifalme. Mungu alimlinda katika tundu la simba.


3️.Petro – Minyororo ilikatika kwa maombi

📖 Matendo ya Mitume 12:5

Kanisa lilikuwa likimwombea Petro kwa bidii gerezani — na malaika akamfungua.


Umuhimu wa maombi.

 Katika maamuzi

Maombi  huleta hekima hivyo Sali na omba upate kufanya maamuzi yenye hekima na busara.

 

 Katika hofu

Maombi huleta amani kati ya hofu ni muhimu kuomba na kusali Mungu akupe amani na ushindi.
📖 Wafilipi 4:6-7

 Katika mahitaji

Maombi huleta majibu, unakumbuka story ya Nabii Elia? Paulo na Sila? Majibu yatakuja tu kwa kufunga na kuomba
📖 Mathayo 7:7

 Katika vita vya kiroho

Maombi ni silaha usiache kuomba.


Mungu hujibu kwa wakati wake.

v Endelea kuomba usiache

Nabii Elia aliomba mara saba bila kuona jibu la haraka.

v Usiangalie ukubwa wa dalili

Wingu lilikuwa dogo kama kiganja cha mkono lakini matokeo yalikua makubwa Zaidi.

v Amini hata kabla hujaona

Kupitia maombi ya Nabii Elia, Mvua kubwa ilikuja baada ya ishara ndogo.


📖 Isaya 40:31
“Wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya.”

Wakati mwingine:

  • Mungu anachelewesha si kwa sababu amekataa
  • Bali kwa sababu anakuandaa

 

Post a Comment

0 Comments